Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Benki ya Dunia anayeshughulikia
Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika Bi. Victoria Kwakwa, tarehe 17
Machi 2025, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Bi. Kwakwa alifika
Ikulu kuaga rasmi baada ya kustaafu kufanya kazi Benki ya Dunia kwa muda
wa miaka 35. Kwa upande wake Rais Dkt. Samia amemshukuru kwa
ushirikiano aliouonyesha kwa Tanzania kwa muda wote wa uongozi wake.