Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akizungumza wakati akifungua kikao kazi kilichowashirikisha wadau wa Gazeti la Serikali kilicholenga kupata maoni kuhusu kusanifu na kujenga Mfumo wa Kidijitali wa Maktaba (POPSM e-Library) kilichofanyika jijini Dodoma.
Na. Mwandishi Wetu-Dodoma
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amesema katika kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi ya TEHAMA Serikalini, Ofisi hiyo imesanifu na kujenga Mfumo wa Kidijitali utakaowawezesha wadau wa Gazeti la Serikali kuwasilisha taarifa zao kwa njia ya kielektroniki.
Katibu Mkuu Mkomi ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi kilichowashirikisha wadau wa Gazeti la Serikali kwa lengo la kuwa na uelewa wa pamoja na kupata maoni yao kuhusu mfumo huo wa kidijitali yatakayosaidia kuboresha ili kuwarahisishia wananchi kuutumia kwa ufasaha.
“Sasa hivi tuko kwenye ulimwengu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ambapo Serikali yetu kupitia Viongozi Wakuu, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekuwa akihimiza mara kwa mara matumizi ya TEHAMA katika utendaji kazi ili kupunguza mianya ya rushwa na gharama, hivyo tunaamini kupitia Mfumo, tutaboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.’’ Amesema Bw. Mkomi.
Bw. Mkomi ameongeza kuwa, Mfumo huo utawawezesha wadau wa Gazeti la Serikali kupata huduma kwa njia ya kielektroniki ambayo ni rahisi, haraka na yenye gharama nafuu itakayowawezesha kuwasilisha taarifa zao zitakazochapishwa na kupatikana kwa Gazeti hilo.
“Sote tunafahamu umuhimu wa Gazeti la Serikali kwa wadau mbalimbali hapa nchini hivyo, kuuboresha mfumo huu kutasaidia sana wadau wetu kuwasilisha taarifa zao kwa haraka na kupunguza malalamiko kama sio kuyaondoa kabisa” Amesisitiza Bw. Mkomi.
Amesema baada ya Ofisi yake kusanifu na kujenga mfumo huo ambao bado ni rasimu, waliona ni vema wakawashirikisha wadau ili kupata maoni yao. Ni matumaini yangu kuwa, kupitia kikao hiki, maoni mbalimbali yatapatikana ili kuboresha mfumo huo ambao ni muhimu kwa wadau wa Gazeti la Serikali.” Bw. Mkomi amesisitiza.
Aidha, ameongeza kuwa, kupitia mfumo huo, taarifa zitahaririwa na kupelekwa kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kwa njia ya kielektroniki.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mary Mwakapenda amewashukuru wadau hao kwa kuitikia wito katika kikao kazi hicho pamoja na maoni mengi waliyoyatoa ambayo yatasaidia katika kuboresha na kuongeza tija katika utekelezaji wa Mfumo huo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akizungumza wakati akifungua kikao kazi kilichowashirikisha wadau wa Gazeti la Serikali kilicholenga kupata maoni kuhusu kusanifu na kujenga Mfumo wa Kidijitali wa Maktaba (POPSM e-Library) kilichofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya wadau wa Gazeti la Serikali wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi kilichowashirikisha wadau hao kwa lengo la kupata maoni kuhusu kusanifu na kujenga Mfumo wa Kidijitali wa Maktaba (POPSM e-Library) kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mary Mwakapenda akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) kuzungumza na wadau wa Gazeti la Serikali wakati wa kikao kazi kilicholenga kupata maoni kuhusu kusanifu na kujenga Mfumo wa Kidijitali wa Maktaba (POPSM e-Library) kilichofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Priscus Kiwango.
Mpigachapa Msaidizi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Kupigachapa, Bw. Silver Chindandi akitoa maoni wakati wa kikao kazi kilichowashirikisha wadau wa Gazeti la Serikali kilicholenga kupata maoni kuhusu kusanifu na kujenga Mfumo wa Kidijitali wa Maktaba (POPSM e-Library) kilichofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya Maafisa wa Maktaba wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi wakati akifungua kikao kazi kilichowashirikisha wadau wa Gazeti la Serikali kilicholenga kupata maoni kuhusu kusanifu na kujenga Mfumo wa Kidijitali wa Maktaba (POPSM e-Library) kilichofanyika jijini Dodoma.
Afisa Ardhi Mwandamizi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Elia Kamihanda akitoa maoni wakati wa kikao kazi kilichowashirikisha wadau wa Gazeti la Serikali kilicholenga kupata maoni kuhusu kusanifu na kujenga Mfumo wa Kidijitali wa Maktaba (POPSM e-Library) kilichofanyika jijini Dodoma.
Wasanifu wa Mfumo wa Kidijitali wa Maktaba (POPSM e-Library) wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi wakati akifungua kikao kazi kilichowashirikisha wadau wa Gazeti la Serikali kilicholenga kupata maoni kuhusu kusanifu na kujenga Mfumo wa Kidijitali wa Maktaba (POPSM e-Library) kilichofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi na wakurugenzi Wasaidizi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakiwa katika kikao kazi kilichowashirikisha wadau wa Gazeti la Serikali kilicholenga kupata maoni kuhusu kusanifu na kujenga Mfumo wa Kidijitali wa Maktaba (POPSM e-Library) kilichofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya wadau wa Gazeti la Serikali wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi kilichowashirikisha wadau hao kwa lengo la kupata maoni kuhusu kusanifu na kujenga Mfumo wa Kidijitali wa Maktaba (POPSM e-Library) kilichofanyika jijini Dodoma.