TIMU ya Polisi Tanzania Ijumaa hii Aprili 18, 2025 inawakaribisha Mbeya City katika mchezo wa Ligi ya Championship, mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Mjini Babati.
Afisa habari wa timu ya Polisi Tanzania Inspekta Frank Lukwaro amesema alama tatu za mchezo huo ni muhimu ikiwemo kulipa kisasi cha kufungwa na Mbeya City katika mchezo wa duru la kwanza katika Uwanja wa Sokoine Mbeya hivyo wameupa umuhimu mkubwa.
Alisema mpaka sasa kikosi hicho kipo vizuri na hakuna majeruhi hivyo kilichobaki ni kuhakikisha kila mchezaji anapambana kuhakikisha wanapata ushindi.
Lukwaro ametoa wito kwa mashabiki wa timu hiyo mjini Babati kujitokeza kwa wingi ili kushirikiana kwa kuwa itakuwa siku ya mapumziko.