Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mkoani Ruvuma Vita Kawawa kushoto,akikabidhi funguo ya Gari la Wagonjwa(Ambulance) aina ya Landcruser kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Namtumbo Jonah Katanga ambalo limetolewa na Serikali kwa ajili ya kituo cha Afya Magazini kata ya Magaazini Wilayani humo.
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Vita Kawawa,akiwasha gari la Wagonjwa aina ya Landcruser lililotolewa na Serikali kwa ajili ya kituo cha Afya Magazini Wilayani humo.
Na Muhidin Amri,Namtumbo
WAKAZI wa vijiji vya Magazini na Lingusenguse wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wameishukuru Serikali kwa kuwaletea gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha Afya cha Magazini kilichopo umbali wa zaidi ya kilomita 230 kutoka Magazini hadi Makao Makuu ya Wilaya ya Namtumbo ambako kuna Hospitali ya Serikali ya Wilaya.
Wakizungumza mara baada Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa
kukabidhi gari hilo aina ya Landcruser kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Namtumbo Jonah Katanga,Wananchi hao wamesema kuwa gari hilo litasaidia kuokoa maisha ya watu kwa kuwapeleka Hospitali kubwa pale wanapotakiwa kwenda Hospitali kubwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Anold Mbunda Mkazi wa kijiji cha Lingusenguse alisema kuwa, walikuwa wanapata adha kubwa kwa wamama wajawazito wanapotaka kwenda hospitali kubwa kwaajiri ya kujifungua wanatembea umbali mrefu zaidi ya kilomita 230 ambako kuna Hospitali ya Serikali.
Ambrose January Jungu(Kaduguda) Mkazi wa Kijiji cha Magazini amemshukuru, Mbunge Vita Kawawa na Serikali kupitia Wizara ya Afya kwani kwa muda mrefu wananchi wa kata ya Magazini wakiwemo akina mama na watoto walikuwa wakisafirishwa kwenye Matenga.
Naye Tizo Matembo mkazi wa kijiji cha Magazini,ameipongeza Serikali kwa kuwapatia gari la kubebea wagonjwa kwani tokea mwanzo walikuwa na matatizo ya usafiri na wagonjwa wengi walifia njiani kabla ya kufikishwa Hospilati ya wilaya kutokana na umbali mrefu na walikuwa wanatumia usafiri wa baiskeli mabo siyo salama.
Kwa upande wake Tabia Nguche Muhudumu wa Afya ngazi ya Jamii kituo cha Magazini alisema awali walikuwa wanapata usumbufu mkubwa hivyo hatua ya Serikali kuwaletea gari la kubebea wagonjwa wakazi wa kata ya Magazini itapunguza changamoto ya muda mrefu ambayo ilikuwa ni kero hasa kwa akina mama wajawazito wanaotaka kujifungua.
Alisema,changamoto hiyo ya usafiri ilipelekea baadhi yao walikuwa wakijifungulia njiani wakati wakisafirishwa kwa matenga kwenda Hospitali ya Wilaya.
Chifu wa kabila ya Wayao Thabiti Nnambi alisema kuwa, hivi karibuni wamepoteza watu zaidi ya kumi ambao walibebwa kwenye matenga wakati wakisafirishwa kwenda Hospitali kwa ajili ya kuopata huduma za matibabu ambapo amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassani na Mbunge wa jimbo la Nambtumbo Vita Kawawa kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuhakikisha kuwa kituo cha Afya Magazine kinapatiwa gari la kubebea wagonjwa.
Mganga Mkuu wa Wilaya Dk. Aron Hyera alisema,kituo cha afya cha Magazini ni kati ya vituo 60 vya kutolea huduma za afya ambacho kipo umbali wa kilomita 230 kutoka Makao Makuu ya Hlamashauri ya Wilaya ya Namtumbo.
Dk. Hyera alisema kuwa, kituo cha Afya cha Magazini kilipokea zaidi y ash. Milioni 500 kwa ajiri ya ujenzi wa majengo 5 ambayo ni jengo la Wagonjwa wa nje, Upasuaji,Maabara,Nyumba moja ya Mtumishi,Jengo la wazazi na chumba cha kuhifadhia Maiti ambapo kituo hicho kina jumla ya watumishi 7sawa na asilimia 13 kati ya 53 ya watumishi wanaohitajika kwa ngazi ya kituo cha afya na kina uwezo wa kuhudumia jumla ya watu elfu 13.
‘’Kituo cha Afya cha Magazini kimepokea sh. milioni 150 kutoka serikali kuu kwaajiri ya ununuzi wa vifaa tiba na vifaa vyote vimepokelewa,,
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Jonah Katanga alisema kuwa halmashauri imetekereza miradi mbalimbali katika kata ya Magazini ikiwemo ujenzi wa kituo cha Walimu,Nyumba za Walimu na miradi mingine ya maendeleo yenye lengo la kuboresha huduma za wananchi.
Naye Mbunge wa Jimbo la Namtumbo vita Kawawa amewaomba watumishi wa kituo cha afya cha Magazini kuona umuhimu wa kulitunza gari la kubebea wagonjwa ambalo litaweza kuwasaidia wakazi a kata ya magazine pale wanapohitaji kwenda hospitali kubwa kwaajiri ya uchunguzi zaidi na akina amama wajawazito wanaopata rufaa kwenda hospitali kubwa kwaajiri ya kujifungua.
Aidha amewataka kutotumia gari hilo kwa manufaa yao binafsi ikiwemo kubebea mafuta,abiria na bidhaa zingine na kuwaomba wananchi wa kata hiyo kuendelea kumuunga mkono Rais Samia na serikali yake kutokana na juhudi mbalimbali anzofanya za kuwaletea maendeleo ikiwemo kuboresha miundombinu kwenye sekta ya afya .