Na Lucas Raphael,Tabora
Bohari ya madawa (MSD) imepongezwa kwa kuzidi kuboresha utoaji huduma kwa wadau wake jambo linalochangiwa na kusikiliza maoni na mapendekezo inayopewa kutokana na vikao vinavyofanywa na MSD na wadau wake.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Tabora na Mkuu wa wilaya ya Tabora Deusdedith Katwale wakati akifungua mkutano wa wateja na wadau wake kanda ya Tabora uliofanyika katika hotel ya JM iliyopo manispaa ya Tabora.
Amesema majadiliano na kukumbushana majukumu ya kila mmoja yamesababisha huduma zinazotolewa na MSD kuwa bora kila siku.
Ameeleza ni lazima ushirikiano uwepo baina ya wateja,wadau pamoja na MSD ili kufikia matarajio ya wananchi kupata huduma bora kutoka MSD ambao ni washirika muhimu katika utoaji huduma za afya.
Amesisitiza ushirikiano miongoni mwa wadau wote wanaoshirikiana na MSD ili hali ya usambazaji vifaa na madawa iwe nzuri zaidi.
“Ili bohari ya madawa ifanikiwe katika utendaji wake wa kazi ni lazima ushirikiane na wadau wake jambo ambalo ni muhimu sana’ amesema
Meneja wa MSD kanda ya Tabora yenye mikoa mitatu ya Kigoma,Katavi na Tabora , Rashid Omary ameeleza kuwa wameongeza usambazaji wa vifaa na vifaa tiba kutoka mara nne hadi mara sita kwa mwaka.
Ameeleza kwa sasa wanatoa huduma kwenye vituo 793 katika mikoa hiyo mitatu ambayo wanapeleka huduma kwa haraka pindi wanapopata mahitaji kutoka kwenye vituo vya kutolea huduma ambapo kwa sasa wanapeleka mara sita kwa mwaka.
Mkurugenzi wa Uendeshaji Victor Sungusia ameeleza kuwa wanaendelea kuboresha utoaji huduma kutokana na Serikali kuongeza fedha na hivyo kufanya huduma kuboreshwa zaidi tofauti na siku zilizopita.
“Kwa wale waliokuwepo miaka ya nyuma watakubaliana nami kuwa huduma zinaendelea kuboreshwa siku hadi siku tofauti na zamani” amesema
Sungusia ameeleza kwamba wana mikakati mingi ya kuboresha huduma ikiwemo kujenga maghala na kuwa na magari mazuri zaidi ambayo yatahifadhi hata joto linalotakiwa kwenye.madawa kuanzia mwanzo hadi wanapoyafikisha kwenye vituo vya kutolea huduma.
Mkutano huo wa siku moja uliokuwa na kauli mbiu “ Tuzungumze Pamoja kutatua changamoto za upatinaji wa bidhaa za afya