Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda (katikati)akitizama magugumajo yaliyotolewa katika ziwa Victoria .

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda akizungumza na baadhi ya wakazi wa kigongo busisi pamoja na abiria waliokuwa wakisubili kuvuka juu ya uondoaji wa magugu maji katika ziwa Victoria

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda akizungumza mara baada ya kukagua zoezi la uondoaji wa magugu maji katika ziwa Victoria
Na Hellen Mtereko Mwanza
Serikali imetoa fedha kwaajili ya ununuzi wa mitambo ya kutokomeza magugu maji katika ziwa Victoria ili yasiathiri shughuli za usafirishaji, uvuvu pamoja na upatikanaji wa maji.
Hayo yamebainishwa leo Jumamosi Mei 10, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kigongo Busisi na waliokuwa wakisubili huduma ya usafiri wa kivuko mara baada ya kuangalia uvunaji wa magugu mapya.
“Leo nimekuja kuangalia uvunaji wa magugu mapya lakini kwaupande wa pili wa daraja kunamsitu mrefu ndani ya ziwa Victoria na hii ni hatari sana kwani maji haya tunayatumia kwaufugaji wa samaki,usafiri na uendeshaji wa maisha yetu ya kila siku”, Alisema Said Mtanda
Alisema utaratibu wa ununuzi wa mitambo hiyo umeshaanza kufanyika na muda si mrefu mitambo mitatu italetwa katika eneo la Kigongo Busisi kwaajili ya kuanza rasmi kusafisha ziwa.
“Feli zetu tatu zilishindwa kufanya kazi ipasavyo kutokana na magugu maji kutokea katika ziwa hili na kwa sasa tunatumia milioni mbili kwa siku kwaajili ya kuwatumia wavuvi wa eneo hili kuyavua magugu maji ili vivuko visiweze kupata changamoto na wananchi waweze kusafiri vizuri na hadi sasa tumevuna tani 600 za magugu maji”, Alisema Mtanda
Aidha, aliongeza kuwa suala la changamoto ya usafiri katika eneo hilo linakwenda kuwa historia kutokana na daraja linaloendelea kujengwa kukamilika hivi karibuni.
Kwaupande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhandisi Cyprian Luhemeja alisema kunamagugu maji ya aina mbili mapya na yazamani.
“Hadi sasa yale mapya angalau yameweza kudhibitiwa ila changamoto ipo kwenye yale ya zamani ambayo tutaanza na hatua ya kwanza ya kuyakata ili kuyapunguzia sipidi ya kukua hatua ya pili Waziri Mkuu alituelekeza tununue mashine za kisasa za kukata ili tuweze kuyaondoa kabisa”, Alisema Luhemeja