NJOMBE, Serikali imemtaka mkandarasi wa kampuni ya LTD Consultant anaejenga mradi wa maji wa miji 28 utakaogharimu kiasi cha 40,425,000,000 kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo ambao utazalisha lita 11 pindi utakapokamilika na kumaliza kabisa changamoto ya mgao na upungufu wa maji Njombe mjini.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Njombe mjini(NJUWASA)Mhandisi Robert Lupoja wakati wa ukaguzi ameweka wazi kwamba mahitaji ya maji ni lita 10,238,500 lakini kinachozalishwa hivi sasa ni lita 5,331,000 na kwamba kukamilika kwa mradi huo kunakwenda kukidhi mahitaji na kuwa na bakaa .
Katika Mradi huo mkandarasi ana jukumu la ujenzi wa mtego wa Maji,Bomba kuu km2.5, Bomba za Usambazaji km40, mtambo wa kutibu Maji pamoja na Tenki la lita 2,000,000.
Baada ya kuona mwenendo wa ujenzi hauridhishi kwenye eneo la bwawa mkuu wa wilaya ya Njombe Juma Sweda akiwa na kamati yake ya ulinzi amemuagiza mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi kwasababu fedha zipo hivyo hategemei kuwepo visingizio katika mradio huo ambao umepewa fedha nyingi na Rais Samia.
Kwa upande wake mkandarasi wa kampuni ya L&T Company Shekh abdul imran na Vmani Nageswararao mshauri wa mradi kutoka kampuni ya
Wapcos LTD consultant wamesema wanakwenda kuchapa kazi kadili wanavyoweza ili ukamilike ndani ya wakati.