Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Mhe. Rachel Kassanda, leo alitembelewa na Nathan Mpangala, Mratibu na Mwezeshaji wa Mradi wa Ufunguo, kwa lengo la kuutambulisha mradi huo na kujadili maandalizi ya warsha ya uchoraji wa komikijamii itakayofanyika kuanzia 14 Julai hadi 22 Agosti mwaka huu. Warsha hiyo inalenga kuwajengea uwezo wachoraji vijana wanaoishi Masasi. Mradi huo umepata ruzuku kutoka Balozi za Uswisi na Norway hapa Tanzania kupitia Programu ya Feel Free Funding inayoratibiwa na Kituo cha sanaa cha Nafasi Art Space.