WAZIRI wa Afya Mhe.Jenista Mhagama,akiwalisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2025 leo Juni 2,2025 bungeni Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
KATIKA kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025 vituo vya kutolea huduma za afya nchini vimeongezeka hadi kufikia 12,846 kutoka vituo 12,266 vilivyokuwepo kipindi kama hicho mwaka 2024 ikiwa ni ongezeko la vituo 580.
Hayo yameelezwa leo Juni 2,2025 na Waziri wa Afya,Jenista Mhagama wakati akiwaslisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Waziri Jenista amesema Wizara imeendelea kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma bora za afya zinazotolewa na watoa huduma wenye weledi na ujuzi, pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya vituo vilivyopo, Wizara imeendelea kujenga vituo vipya ili kuleta huduma karibu na wananchi.
Amesema katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025 vituo vya kutolea huduma za afya nchini vimeongezeka hadi kufikia 12,846 kutoka vituo 12,266 vilivyokuwepo kipindi kama hicho mwaka 2024 ikiwa ni ongezeko la vituo 580.
Amesema Kati ya vituo 54 hivyo 12,846, Vituo vya umma vilikuwa 7,627 na binafsi ni 5,219.