*Miradi yote ya maendeleo yapitishwa na Mwenge wa Uhuru 2025 hakuna mradi uliokataliwa.
Mwenge wa Uhuru 2025 unaendelea kukimbizwa katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo katika Wilaya ya Ilala miradi 7 yenye thamani 44,361,798,122.55 imepitishwa na Mwenge wa Uhuru hakuna mradi uliokataliwa.
Aidha katika miradi hiyo Mwenge wa Uhuru umetembelea, umekagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa Nishati Safi Soko la Samaki Ferry, Ujenzi wa barabara ya Magengeni Chang’ombe, Mradi wa Vijana 4% kikundi cha Ulipo Tupo, Mradi wa Usambaji maji Bangulo, Kituo cha afya Ukonga, Kituo cha Polisi Ukonga na Shule ya Sekondari Ukonga.
Mwenge wa Uhuru 2025 leo Juni 4, 2025 unaendelea Wilaya Kinondoni ambapo utatembelea, utakagua, kuweka Jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.