Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .VIONGOZI wa dini wametakiwa kuendelea kulinda amani ya nchi pamoja na kuiombea nchi pamoja na viongozi wake pamoja na kuacha tofauti zao na kuwa kitu kimoja katika kufanya yale waliyoitiwa .
Hayo yamesemwa wilayani Arumeru mkoani Arusha na Mjumbe wa kamati kuu CCM na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga,Rajab Abdarahim wakati akizungumza katika mahafali ya 85 ya wahitimu katika chuo cha biblia Sakila kilichopo wilayani Arumeru mkoani Arusha ambapo jumla ya wahitimu 66 wamehitimu ngazi ya stashahada chuoni hapo.
Amesema kuwa, viongozi wa dini wanatakiwa wawe mfano wa kuigwa katika jamii na sio kuwa sehemu ya kuchochea migogoro kwani hiyo sio kazi waliotumwa kufanya .
“Nyie kama viongozi wa dini mnatakiwa mtumike ipasavyo katika kuhubiri injili na kuhakikisha mnaombea nchi inakuwa na amani pamoja na viongozi wake kwani hilo ndilo kusudi lenu na sio vinginevyo”amesema Hashim.
“Naombeni sana mhakikishe mnaombea nchi yetu ili.izidi kuwa na amani pamoja na Rais wetu aliyeko madarani kwani Tanzania imekuwa ni nchi ya amani muda mrefu na wenzetu wanaitamani sana hii amani tuliyonayo na wakuhakikisha hii amani inakuwepo ni nyie kuendelea kuzidisha maombi.”amesema .
Aidha amewataka wahitimu kuhakikisha wanakuwa mbegu ya kwenda kukitangaza chuo hicho pamoja na kuyaishi yale yote waliyofundishwa pamoja na kuyaishi malezi bora waliyoyapata hapo chuoni .
Kwa upande wake Askofu mkuu wa makanisa ya International Evangelism Tanzania ,Askofu Dkt. Eliud Issangya amesema kuwa ,amekemea vikali tabia ya watu wanaotukana viongozi kwani kwa kufanya hivyo wanajisababishia laana kwani sasa hivi sio wakati wa kutukana viongozi bali wanapaswa kuwaombea wao na Taifa kwa ujumla ili Mungu azidishe amani.
“Haiwezekani Rais wetu atukanwe na sisi viongozi tunakaa kimya ila kinachotakiwa ni kuhakikisha tunaomba na kuacha mdomo ,kamwe tusitukane viongozi wetu bali tuwaheshimu viongozi waliopo madarakani ili.siku zetu zipate kuwa nyingi hapa duniani.”amesema .
“Sisi kama viongozi wa dini kazi tuliyoitiwa ni kuhakikisha tunaombea nchi yetu ili.an9 izidi kudumu huku tukiwaombea na viongozi waliopo madarakani ili waweze kuongozwa na roho wa Mungu “amesema .
Naye mmoja wa wahitimu akisoma risala amesema kuwa ,wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu mibovu ya barabara kutoka Kikatiti hadi Sakila ambapo wameombwa kiwekwe kiwango cha Lami kwani wakiweka.Lami biashara zitaweza kufanyika kwa wingi.
“Sisi kama vijana tunapenda kutoa angalizo kwa baadhi ya watu wanaomshambulia Rais Samia kuacha mara moja tabia hizo kwani hicho ni kitendo kibaya sana na hakitakiwi kabisa kwa viongozi badala yake wanatakiwa wawaheshimu na kuwaombea .”amesema .