NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma maarufu kwa jina la FA amebainisha kuwa timu ya Tanzania ipo vizuri. Hayo alisema mara baada ya Tanzania kupata ushindi dhidi ya Uganda. Mwinjuma amesema kwenye mpira wa miguu lolote linaweza kutokea.
Ikumbukwe kwamba kwenye mashindano maalumu ya CECAFA ambayo yalishirikisha timu tatu, Tanzania, Uganda na Senegal bingwa ni Tanzania.
Katika mchezo wa Julai 27 2025 uliochezwa Uwanja wa Black Rhino baada ya dakika 90 Tanzania ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Senagal.
FA alisema: “Timu ipo tayari sijaona timu nyingi zikishiriki.Ila kwa timu ambazo zimeshiriki Uganda na Senegal nit imu nzuri. Kwa sasa tuna nafasi kitwakimu kuchukua ubingwa huu.
“Kupata matokeo mbele ya Uganda, Senegal hapo unaona kwamba tumechukua CHAN ya huku Karatu. Bado CHAN 2024 ya Afrika nzima ambayo tunakwenda kushiriki. Tuna nafasi kubwa kuchukua kombe hili kuliko wakati wowote ule ila kwenye mpira lolote linaweza kutokea,”.