WAKATI akitajwa kuwa huenda anaweza kuwa nyeupe na nyekundu kiungo mkabaji Khalid Aucho inaelezwa kuwa mpango huo ni ngumu kukamilika.
Tetesi zimekuwa zikieleza kuwa Simba SC inahitaji huduma ya Aucho ambaye mkataba wake umegota mwisho ndani ya Yanga SC msimu wa 2024/25.
Kwa sasa ni mchezaji huru na amewashukuru Yanga SC na mashabiki kwa kuwa naye bega kwa bega nyakati zote hizo alipokuwa na uzi wa kijani na njano.
Aucho msimu wa 2024/25 kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika alihusika kwenye mabao mawili, alifunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.
Taarifa zinaeleza kuwa mchezaji Aucho kwa sasa hayupo tayari kucheza ndani ya Tanzania kwa timu nyingine nje ya Yanga SC hivyo atakwenda kupata changamoto nje ya Bongo.
Kwa maana hiyo ikiwa Simba SC wanahitaji saini ya Aucho kwa msimu wa 2025/26 itakuwa ngumu kwao kuipata kulingana na mipango ya mchezaji mwenyewe kwa sasa.