TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefungua pazia la CHAN 2024 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burkina Faso mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa Agosti 2 2025 mbele ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia burudani hiyo.
Mabao yamefungwa na Sopu dakika ya 45 kwa mkwaju wa penalti iliyosababishwa na Clement Mzize katika mchezo wa kundi B huku Tanzania wakiongoza kundi na pointi 3.
Bao la pili limefungwa na Mohamed Hussen Zimbwe Jr dakika ya 74 akitumia pasi ya Mudathir Yahya ambapo bao hilo liliamuriwa na VAR, Uwanja wa Mkapa.
Mchezaji bora wa mchezo wa CHAN 2024 ni Feisal Salum huku Yusuph Kagoma akiingia kwenye orodha ya wachezaji walioonyeshwa kadi ya njano.
Kipa wa Burkina Faso alionyesha ubora dakika 90 kwa kuonyesha kazi kubwa katika kuokoa hatari za wachezaji wa Stars ikiwa ni Dickson Job, Sopu na Job.
Umiliki ilikuwa ni asilimia 60.3 kwa Tanzania na 39.7 kwa Burkina na kona zilipigwa 7 kwa Tanzania na Burkina Faso hawakupata kona.
Baada ya ushindi huo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo, Prof. Palamagamba Kabudi aliikabidhi Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) shilingi milioni 20 (Goli la Mama) baada ya kuifunga Burkina Faso 2 – 0 katika ufunguzi wa Mashindano ya CHAN Agosti 2, 2024 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Fedha hizo zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kama alivyoahidi kila goli moja shilingi milioni kumi.
Pia Prof. Kabudi nae alitoa shilingi milioni 20 pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ambaye alitoa kiasi cha Milioni 20.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata