“Mdogo wangu Hansi Rafaeli nimeona andiko lako umenipopoa kuwa napambana kuzima utambulisho wa Zimbwe, kwakua umemtaja Zimbwe hili siwezi kujibu maana umemtaja mtu ninaemuheshimu na kumpenda sana.
Lakini kwakua umenivaa maungoni nami siwez kufunika kombe
Kwanza naomba nikuulize tuu hii vita ni yako binafsi au umetumwa na wale wanaoliliana harusini
Kama wamekutuma basi wamekubebesha mzigo mkubwa sana mdogo wangu
Hao wenzio wameshanishindwa hawaniwezi na wananiogopa kama Mjumbe wa CCM
Wameshanishtaki saaaana, Wamenishtaki TFF na nikawabwaga vibaya vibaya
Sasa wamekuongeza na wewe hakikisha umejipanga maana umekaa upande dhaifu
Kingine ninachoomba kujua tu unataka vita na mimi kama Mwandishi au Wakala mtiifu wa kikundi cha kuliliana harusini
Ni muhimu nijue haya ili nikishambulia nijue namshambulia adui wa aina gani?
Ukiwa unasimama kama Mwandishi basi niache kukushambulia maana kawaida yangu naheshimu sana Waandishi na tena naheshimu sana Media yako hivyo siwezi kukujibu.
Ila kama umekaa upande wa wapinzani wangu jipange mdogo wangu mimi sio mtu wa kawaida!!” Ameandika Msemaji wa Simba -Ahmedy Ally.