Klabu ya Singida Black Stars imetangaza rasmi kuwa tamasha lao la kila mwaka la ‘Singida Big Day’ litafanyika mwaka huu kwa mara ya kwanza jijini Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, tarehe 6 Septemba 2025.
Black Stars wanafanya tamasha hilo nje ya Singida ni kufuatia ukarabati unaoendelea katika uwanja wa Airtel Stadium na CCM LITI mkoani Singida pamoja na lengo la kupanua wigo wa mashabiki wa timu hiyo kutoka kanda ya Kaskazini na kuimarisha hadhi ya Singida Black Stars kitaifa.
Tamasha hilo litafanyika matukio muhimu kama utambulisho wa kikosi kipya cha Singida Black Stars pamoja na ripoti ya usajili wa msimu wa 2025/26 na mechi ya kirafiki kati ya Singida Black Stars na timu ya kimataifa.