MZIZE NJE, EDMUND NDANI.
Klabu ya Yanga imekamilisha Usajili wa Kiungo Mshambuliaji wa Singida Black Stars Edmund John ambaye anakuja Kuchukua nafasi ya Clement Mzize ambaye ataondoka Yanga baada ya michuano ya CHAN 2024.
Katika msafara wa wachezaji wa Yanga uliotua katika uwanja wa Ndege wa Kigali Rwanda nyota huyo ameonekana akiwa na kikosi hicho.
Edmund John anatarajiwa kutangazwa kama mchezaji Mpya wa Yanga katika Tamasha la RAYON DAY Linalotarajiwa kufanyika August 15 katika Dimba la Amahoro Stadium
Klabu ya Esperance ya Tunisia inatajwa kuwa katika hatua za mwisho za kukamilisha uhamisho wa Mzize.