NANTES: Kocha wa Mabingwa wa Ulaya Paris St Germain, Luis Enrique, amsema anafurahishwa na maendeleo ya wachezaji wake ndani ya wiki moja ya mazoezi baada ya mapumziko yenye shughuli nyingi walipomaliza washindi wa pili wa Kombe la Dunia la klabu na anaamini wanaweza kutetea taji lao la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
PSG wamekuwa na vipindi vifupi vya mazoezi kabla ya kutwaa taji la UEFA Super Cup mbele ya Tottenham Hotspur kwa mikwaju ya penalti usiku wa Jumatano, huku Luis Enrique akisifu ari ya kupambana ya timu yake wakati huu wanapoanza harakati za kuwania taji la tano mfululizo la Ligue 1.
“Napenda jinsi timu ilivyopambana Kwenye Super Cup, hasa kwa mazoezi kidogo. Hiyo imekuwa DNA ya timu hii katika misimu ya hivi karibuni, inapambana kila wakati,” – Enrique aliwaambia waandishi wa habari kuelekea mechi ya kwanza ya Ligue 1 dhidi ya Nantes.
“Tunachotaka sasa ni kurudisha hisia zetu kwenye mpira kwa sasa ni kawaida kutokuwa timamu kwa 100%.
Luis Enrique, ambaye ameshinda mataji mfululizo ya ligi akiwa PSG, awali aliiongoza Barcelona kutwaa mataji mawili ya LaLiga mfululizo.
Alipoulizwa kuhusu lengo kuu la PSG msimu huu, Mhispania huyo alisema anataka kushinda tena Ligi ya Mabingwa baada ya kuicharaza Inter Milan mabao 5-0 kwenye fainali msimu uliopita.
The post Enrique aota tena ubingwa UCL first appeared on SpotiLEO.