LONDON, MENEJA wa Crystal Palace Oliver Glasner amesema wachezaji Eberechi Eze na Marc Guehi wote wataanza kwa katika mechi yao ya kwanza ya ‘playoff’ ya UEFA Conference League leo usiku licha ya kuhusishwa pakubwa kuondoka klabuni hapo msimu huu.
Mshambuliaji Eberechi Eze anatakiwa na Tottenham Hotspur na Arsenal huku mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Uingereza Marc Guehi akivutiwa na mabingwa wa Ligi Kuu ya England Liverpool.
Wote walicheza katika sare ya 0-0 ya Palace na Chelsea katika mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi na meneja Oliver Glasner hana wasiwasi kuwachezesha tena dhidi ya Fredrikstad ya Norway usiku wa leo Alhamisi.
Eze alifunga bao la ushindi dhidi ya Manchester City katika fainali ya Kombe la FA na kuifungia Palace safari yake ya kwanza kwenye michuano ya Ulaya, ingawa ni kwenye Conference League badala ya Europa, na anasalia kuwa mtu mashuhuri zaidi klabuni na kwa mashabiki.
“Mchezaji anajitoa 100% kwa sababu yuko chini ya mkataba. Sio lazima tutoe ‘Thank you’ kila siku. Wengi mlishangaa yeye na Marc (Guehi) kuanza dhidi ya Chelsea, unaweza kushangaa wakaanza tena, lakini mpaka sasa wamejitoa sana kwa ajili ya timu.” – Glasner aliwaambia wanahabari Jumatano.
“Watakuwa na jukumu muhimu kwa muda wote wakiwa hapa wamejitolea kwa timu. Ikiwa wataondoka, wanataka kuondoka kama vijana ambao walitoa 100% kwa Crystal Palace.”
The post Eze, Guehi kukichafua Conference League first appeared on SpotiLEO.