MTANDAONI; Chati ya Apple Music Tanzania Top Albums ya mchana huu imeonesha mabadiliko makubwa, ikidhihirisha ushindani mkali kati ya wasanii wa kimataifa na wa ndani.
Albamu mpya ya Offset, “Kiari”, iliyotolewa, imepanda kwa kasi hadi nafasi ya kwanza, na kumpiku Mbosso ambaye alikuwa ameongoza kwa zaidi ya miezi miwili mfululizo kupitia albamu yake “Room Number 3”.
Wasanii wengine pia wameingia kwa nguvu kwenye chati hiyo. Msanii chipukizi Yammi, kupitia EP yake mpya “After All”, ambayo pia ilitoka jana, amejiweka kwenye nafasi ya nne, akionyesha kupokelewa vizuri na mashabiki.
Wakati huo huo, baadhi ya kazi kutoka kwa wasanii wa Tanzania zimeanza kuporomoka taratibu. EP ya “Time” kutoka kwa Lava Lava na albamu ya “KitaaREJEX” ya rapa mkongwe Fid Q zimepoteza nafasi kadhaa. Hata hivyo, Chris Brown anaendelea kushikilia nafasi ya juu kupitia albamu yake “11:11 (Deluxe)”, ambayo imekuwa ndani ya Top 10 kwa takriban mwaka mzima.
Pamoja na mafanikio haya ya kimataifa, chati hii inaonesha changamoto kwa muziki wa Bongo Fleva kwenye jukwaa la kimataifa.
Ni albamu au EP nne tu kutoka kwa wasanii wa Tanzania ndizo zinazoonekana ndani ya kumi bora hali inayoweza kufungua mjadala kuhusu mwelekeo wa usikilizwaji wa muziki wa ndani dhidi ya wa nje kwenye majukwaa ya kidijitali kama Apple Music.
The post Mabadiliko makubwa kwenye chati ya apple Music first appeared on SpotiLEO.