MANCHESTER: MENEJA wa Manchester United Ruben Amorim amelaumu hisia zake kwa kauli yake baada ya mechi waliyopoteza dhidi ya Grimsby, kauli zilizozua taharuki na maswali kwa mashabiki kuhusu mustakabali akisema “wakati mwingine natamani kuacha”.
Mara tu baada ya kufungashiwa virago kwenye Kombe la Carabao na timu ya Ligi Daraja la Pili (League Two) usiku wa Jumatano, Mreno huyo alisema timu yake “imepotea kabisa” na kwamba “kuna kitu lazima kibadilike”.
Aliamua kutofafanua maoni yake hayo, ambayo hata ndani ya Old Trafford yametafsiriwa na wengi kama hatua ya karibu ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 40 kutojua mustakabali wake ndani ya United.
Lakini akizungumza mapema leo Ijumaa, amesema:
“Kusema kweli, kila wakati tunapopoteza mchezo kwa staili ile siku zijazo lazima nitakuwa vile. Nitasema wakati mwingine nawachukia wachezaji wangu na wakati mwingine nawapenda. Wakati mwingine nataka kuacha kazi, wakati mwingine nataka kuwa hapa kwa miaka 20”. – amesema Amorim
The post “Kuna wakati natamani kuiacha United” – Amorim first appeared on SpotiLEO.