DAR ES SALAAM: MSANII nyota wa Bongo Fleva, Mbwana Kilungi maarufu kama Mbosso Khan, amesema hana cha kuwalipa mashabiki wake kufuatia mafanikio makubwa ya wimbo wake Pawa, ambao umefikisha watazamaji milioni 30 ndani ya miezi miwili tu tangu kuachiwa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mbosso ameonesha hisia za shukrani kwa mashabiki waliounga mkono kazi yake kwa upendo mkubwa, huku akiandika:
“Milioni 30 ndani ya miezi 2… Nitawalipa nini jamani kwa huu upendo?”
Wimbo wa Pawa umeendelea kutikisa anga la muziki wa Afrika Mashariki, huku ukimpa msanii huyo mafanikio zaidi kimuziki na kumpa nafasi ya kuendelea kuangaza katika tasnia ya muziki.
Mashabiki na wadau wa muziki wameendelea kumpongeza Mbosso kwa kazi nzuri na kuahidi kuendelea kumuunga mkono katika safari yake ya muziki.
The post Pawa yafanya maajabu YouTube first appeared on SpotiLEO.