Staa wa muziki wa bongefleva Mbosso Khan amewashukuru mashabiki,wanachama na viongozi wa Simba kwa kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye tamasha la Simba Day huku akiweka wazi almanusura apoteze uhai wake.
“Barua Kwa Uongozi na Mashabiki Wa Simba Sports Club @simbasctanzania
Asanteni Sana Kwa kuniamini na kwa kunipa nafasi hii adhimu ambayo mngeweza kumpa mtu yoyote mumtakae na badala yake mkanichagua mimi kuwa headliner wa tamasha hili kubwa la kihistoria SIMBA DAY.
Kwangu mimi hili ni tamasha langu kubwa la kwanza kuwahi kulifanya la uwanjani linalohusiana na mpira wa miguu katika maisha yangu ya mziki , ndo maana nilichagua kufanya kila lililo ndani ya uwezo wangu ili kuhakikisha nawapa furaha mashabiki na wadau wa Simba Sports Club
Ndo Maana Kwangu halikuwa tu tamasha, bali niliona kama Platform Ya Kuonyesha Sehemu Ya Vipaji Ambavyo Mwenyezi Mungu Amenijaalia na pengine hamkuwahi kuviona hapo awali mfano Kuigiza kwa Uhalisia Wa Daraja la Juu , kuimba na Vengine ambavyo Viliwavutia.. ( Almanusuru Nitoe Uhai Kwenye Kuandaa Furaha Kwa Wana Simba )
Siwezi Kusema ni kiasi gani cha Pesa nimetumia kwenye hili ila fahamu kila nilichofanya ni kwa Sababu Ya Mapenzi Yangu Makubwa na Club Yangu Hii Pendwa Ya Simba Sports Club
Nina imani Mlifurahi Na Kama kuna Sehemu nilikosea au Palikuwa na Mapungufu Naomba Mnisamehe Sababu Mimi ni Mwanadamu Siwezi Fanya Vyote Kwa Ukamilifu”