Kocha Mkuu wa Simba amezungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho wa dabi ya kariakoo huku akiweka wazi hawana presha ya mchezo huo ila Yanga ndiyo wenye presha.
“Sisi tuna faida ya kuwa na benchi lilelile la ufundi lakini tuna wachezaji wapya ambao tunao kwa wiki kama tatu hadi nne na tumekuwa na mazoezi ya pamoja kwa siku chache na waliopo CHAN hivyo naamini tuko vizuri.
Lakini presha kubwa ipo kwa Yanga kwasababu wana makocha wapya ambao hawajawahi kucheza hii dabi lakini pia presha ya muendelezo wa matokeo yao lakini kwetu hatuna presha kwasababu benchi ni lile lile na wachezaji wapya wanaonekana kuuhitaji mchezo tukichanganya na wazoefu tutakuwa na ‘balance’ nzuri” – Fadlu Davids, Kocha Simba SC