MAREKANI:MSANII mrembo na mwanamitindo maarufu duniani, ambaye pia ni mfanyabiashara mwenye mafanikio, Robyn Rihanna Fenty ‘Rihanna’, amemtambulisha kwa mara ya kwanza mtoto wake wa tatu kupitia picha ya kipekee iliyopigwa Septemba 13, 2025.
Rihanna, ambaye amekuwa nje ya macho ya umma kwa kipindi kifupi, amethibitisha kwamba alijifungua mtoto huyo tarehe 13 Septemba mwaka huu.
Mtoto huyo wa kiume amepewa jina la Rocki Irish Mayers, akiendeleza utamaduni wa majina ya kipekee ndani ya familia ya Rihanna na mpenzi wake, rapa ASAP Rocky.
Wawili hao tayari wana watoto watatu: RZA, mwenye umri wa miaka mitatu, na Riot, ambaye ana umri wa miaka miwili na mdogo wao sasa.
Hii inaifanya familia yao kuwa na watoto watatu, na kuzidi kuonesha uimara wa uhusiano wao wa muda mrefu.
Mashabiki duniani kote wamepokea habari hizo kwa furaha, huku picha ya mtoto huyo ikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.
The post Rihanna amuweka wazi mtoto wake wa tatu first appeared on SpotiLEO.