DAR ES SALAAM:MALKIA wa muziki wa injili nchini Tanzania, Rose Muhando, amefunguka kuhusu mafanikio makubwa aliyoyapata kupitia wimbo wake maarufu “Nibebe”, akisema kuwa ni miongoni mwa nyimbo zilizomletea fedha nyingi zaidi katika maisha yake ya muziki.
Akizungumza kwa furaha, Rose amesema kuwa “Nibebe” si tu wimbo wa kiroho, bali pia ulikuwa baraka ya kiuchumi kwake.
“Nibebe ilinifanya nikanunua Prado. Niliwahi kulipwa milioni tano za Kenya kwa mara moja.Ni sawa na zaidi ya milioni100 kitanzania,” amesema Rose.
Rose Muhando, ambaye ameendelea kutikisa anga la muziki wa injili kwa miaka mingi, amesema licha ya kuwa na nyimbo nyingi zinazopendwa, “Nibebe” ni wimbo anaouenzi sana kutokana na mafanikio yaliyokuja nayo.
Hii ni ishara kuwa muziki wa injili, licha ya kuwa na ujumbe wa kiroho, pia unaweza kuwa chanzo cha mafanikio ya kifedha kwa wasanii wanaoutumikia kwa moyo wa dhati.
Je, ni wimbo gani unaupenda kutoka kwa Malkia Rose Muhando? “Nibebe” ni miongoni mwa nyimbo zako pendwa, au kuna mwingine unaukubali zaidi?
The post Wimbo wa “Nibebe” ulimpa mamilioni Rose Muhando first appeared on SpotiLEO.