NEW YORK: MWIMBAJI huyo mwenye umri wa miaka 34 ambaye alijipatia umaarufu mwaka 2012 aliposhiriki katika kipindi cha ‘DJ Fresh’s Hot Right Now’ ameweka wazi kwamba ataachia filamu itakayohusu maisha yake ndani ya miaka nane.
Rita aliliambia The Sun: “Nimekuwa nikijirekodi kwa miaka minane iliyopita na siku moja nitalazimika kutumia picha hizo kuelezea nilichokifanya kwa miaka nane.
“Nimekuwa na vyumba vya kubadilishia nguo vikijaa, vazi langu halijafika kwa wakati. Wakati mwingine sikuwa na msanii wa kujipodoa na imenibidi kujificha chini ya miwani yangu ya jua.” Amesema Rita huku yote hayo akitaraji kuyaonesha katika fila,u hiyo.
Rita na mumewe, mkurugenzi Taika Waititi, kwa sasa wanaandaa wimbo kulingana na Tamasha la Fyre 2017 na wanataraji kufunguliwa London na New York.
Mume wa Rita alisema: “Kwa kweli ilikuwa ni lazima kumfanya afanye video hii, na ilikuwa nzuri sana kwamba aliacha kila kitu na kufanya hivyo.”
Rita alieleza: “Inachekesha sana. Nilikuwa nikirekodi, na ni wazi mpiga picha lazima afanye picha za kuzunguka digrii 360.
“Ameweka kamera hii na anapiga, na Taika alikuwa anaimba, ‘Shoot the bum, shoot the bum’ siku moja nitaiachia filamu hiyo yenye matukio yangu mengi ya kushangaza na kuchekesha” alimaliza Rita.
The post Rita Ora kutoa filamu miaka 8 ya maisha yake first appeared on SpotiLEO.