Klabu ya Simba SC imetoa shukrani kwa Kocha Hemed Suleiman maarufu Morocco kwa kuiongoza timu hiyo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na kufanikisha kutinga hatua inayofuata.
Simba pia imelishukuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kumruhusu Kocha Morocco, ambaye ni Kocha wa Taifa Stars, kuungana na kikosi hicho kwa ajili ya mchezo huo muhimu uliokuwa na presha kubwa ya ushindani.
Aidha, Simba imesema mchakato wa kumpata kocha mpya wa kudumu uko katika hatua za mwisho na hivi karibuni watamtambulisha rasmi kwa mashabiki na wanachama wao.
Baada ya mechi jana Morocco alipohojiwa na Mtangazaji wa Crown Media kama ataendelea kubaki Msimbazi alikataa kuongelea jambo hilo akieleza kuwa yeye ni kocha wa Stars pekee.