Beki Rushine De Reuck amefunga bao lake la pili la msimu na kuwa kinara wa magoli akiwa na magoli mawili sawa na Paul Peter wa JKT Tanzania na Faisal Salum ‘Feitoto’ wa Azam FC
Akizungumza amesema “Kwangu mimi ushindi wa timu ndio jambo muhimu, kuhakikisha tunafikia malengo na mafanikio ya juu, Sijui ni bahati tu kuzipata nafasi za kufunga ila lengo ni kuleta ushindi kwenye timu na nafasi ikipatikana unajarib kuitumia” Alisema Rushine De Reuck.
Lakini pia Selemani Mwalimu ‘Gomez’ amefungua akaunti yake ya magoli kwenye Ligi Kuu bara msimu wa 2025/26 wakati Simba Sc ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Namungo Fc katika dimba la Benjamin Mkapa kukwea kileleni alama 7 baada ya mechi mbili.