Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Prince Dube, anaripotiwa kuwa katika mawazo mazito ya kustaafu soka, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa rafiki yake wa karibu.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa Dube amekuwa akipitia kipindi kigumu ndani na nje ya uwanja, huku kasi yake ya kupoteza ubora ikionekana wazi katika mechi kadhaa zilizopita.
Inadaiwa kuwa nyota huyo kutoka Zimbabwe amefikia hatua ya kuhisi kuwa amerogwa, jambo lililoongeza zaidi msongo wa mawazo kwake.
Dube, ambaye amewahi kuwa miongoni mwa washambuliaji hatari katika Ligi Kuu Tanzania Bara, amekuwa akikosa kujiamini, na mara kadhaa kuonekana mwenye huzuni.
Hadi sasa, uongozi wa Yanga haujatoa tamko rasmi, lakini taarifa zinaeleza kuwa baadhi ya viongozi wanajaribu kumshawishi mchezaji huyo abadili mawazo na kuendelea kupigania nafasi yake.









