Kocha wa zamani wa Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania,Jamhuri Kihwelu Julio ameitaja Klabu ya Yanga kuwa ina uwezo wa kufanya lolote kwenye kundi lake la Klabu bingwa Afrika lenye Klabu za Al Ahly,As Far Rabat na Js Kabylie.
Julio amesema Yanga wanao uwezo na huu sio muda wa kuwa na hofu na wapinzani kutoka Kaskazini kwani tayari wameshazifunga Klabu za ukanda huo kwa miaka ya karibuni.
Kocha huyo amesema Yanga inaweza kufanya vizuri zaidi pengine hata kuliko Simba inayopewa chapuo la kufuzu kwenye kundi lake.
Je hii ni kauli ya faraja au ni uhalisia?
The post Kocha Julio “Yanga Wamepangwa Kundi Jepesi, Watakinukisha Kuliko Simba” appeared first on Soka Tanzania.




