MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema mchakato wa kuunda benchi imara la ufundi unaendelea kwa umakini mkubwa, na kufikia Desemba 28 kocha mpya atakuwa ameshapatikana rasmi.
Amesema katika tarehe hiyo hiyo timu itarejea kambini, na tayari kocha mpya atakuwa ameanza programu zake za kuandaa kikosi kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.
Kwa mujibu wa Ahmed, makocha kutoka mataifa mbalimbali wametuma maombi ya kujiunga na Simba, lakini uongozi unaendelea kuchambua majina ya waliolengwa, wakiwamo wale walio na mikataba katika klabu nyingine.
Amesisitiza kuwa mchujo huo unafanywa kwa umakini ili kupata mwalimu ambaye ataendeleza kazi iliyoachwa na benchi lililopita.
Amewatoa hofu mashabiki na kuwataka kupunguza presha kutokana na taarifa zinazozungumzwa mitandaoni, akiwataka kuwaamini viongozi wao ambao wapo kwa ajili ya kuhakikisha Simba inabaki imara na yenye ushindani.
Ahmed ameongeza kuwa baada ya kuachana na Meneja Dimitar
Pantev, uongozi unaendelea kuimarisha benchi la ufundi kwa kusimamia upatikanaji wa kocha mpya kulingana na tathmini ya michezo ya Ligi Kuu na michuano ya kimataifa ambayo tayari klabu hiyo imecheza msimu huu.
The post HATUTAFUTI KOCHA KWA MIHEMKO, AHMEDY ALLY appeared first on Soka La Bongo.








