Nigeria vs Tanzania ni mchezo mkali unaosubiriwa kwa shauku kwenye mashindano ya AFCON 2025 ikiwa ni hatua ya makundi nchini Morocco.
Tayari mchezo wa ufunguzi ulishachezwa rasmi Desemba 21 ya Jumapili na wenyeji Morocco wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Comoros.
Leo ni kazi ya wawakilishi kutoka Tanzania, Taifa Stars wakiongozwa na nahodha Mbwana Samatta ambaye yupo nchini Morocco.
Ni Nigeria vs Tanzania miongoni mwa kazi ngumu kwa wababe wote wawili ikiwa ni hatua ya makundi.
Miguel Gamondi anatarajiwa kuchanga karata yake ya kwanza leo katika kampeni ya kuwania kufuzu hatua ya robo fainali.
Jumanne, Desemba 23, 2025
Congo Dr vs Benin, saa 9:30 alasiri
Senegal vs Botswana, saa 12:00 jioni
Nigeria vs Tanzania, saa 2:30 usiku
Tunisia vs Uganda, saa 5:00 usiku.





