MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally, ameonesha imani kubwa kwa benchi jipya la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Steve Barker amesisitiza kuwa matarajio ya uongozi na mashabiki ni makubwa kutokana na ubora wa benchi hilo.
Ahmed amesema benchi hilo limeundwa na wataalamu wenye uzoefu na uwezo mkubwa wa kuiongoza Simba katika ushindani wa ndani na kimataifa, hali inayoongeza matumaini ya kufanya vizuri katika mashindano yanayoendelea na yajayo.
Ameeleza kuwa mabadiliko yaliyofanywa kwenye benchi la ufundi yamelenga kuimarisha falsafa ya timu, kuongeza ushindani ndani ya kikosi pamoja na kuboresha kiwango cha wachezaji mmoja mmoja na kwa ujumla wa timu.
“Uongozi wa klabu umejipanga kikamilifu kutoa ushirikiano na mazingira bora kwa benchi jipya la ufundi ili liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kufikia malengo yaliyowekwa,” amesema.
Ahmed amewataka mashabiki na wanachama wa Simba kuendelea kuwa na subira na imani, kuwa mafanikio yanahitaji mshikamano, uvumilivu na kuamini mchakato unaoendelea ndani ya klabu.
Ameongeza kuwa benchi jipya la ufundi lina kiu ya mafanikio na dhamira ya dhati ya kuirejesha Simba katika ubora wake, klabu itaendelea kupambana kuhakikisha ndoto za mashabiki wake zinatimia.
The post SIMBA SC IMANI KUBWA BENCI LA UFUNDI appeared first on Soka La Bongo.





