SHIRIKA la Petroli Tanzania (TPDC) limetoa ufafanuzi juu changamoto iliyojitokeza hivi karibuni ya kuwepo kwa msongamano wa magari kwenye vituo vya kujazia gesi ya CNG vilivyosababishwa na changamoto ya hitilafu ya umeme kwenye kituo cha Uwanja wa ndege
Akizungumza na waandishi wa habari leo Octoba 3,2024 Kaimu Mkurugenzi wa biashara ya petroli na gesi Emmanuel Girbert amesema uhitaji wa gesi ya CNG kwa sasa nchini ni mkubwa hivyo miundombinu iliyopo inapaswa kuongezwa ili kukidhi mahitaji.
“Tumeanza kutumia gesi ya CNG miaka ya hivi karibuni na tukiwa na kituo chetu kimoja cha ubungo lakini hivi sasa mahitaji ni makubwa sana kwani mpaka sasa hivi tunavituo vitatu ambapo kituo kimoja ni kituo dada ambacho kinategemea kutuo mama ambacho mfano wa kituo dada ni kile cha Tazara ambacho kinategemea kituo cha Ubungo”,Amesema
Aidha amesema mpaka sasa kuna magari takribani 4500 ya CNG na vituo vilivyopo uwezo wake ni kujaza magari 1200 mpaka 1500 kwa siku.
“TPDC kwa kuona hadha hiyo tukaona sisi wenyewe hatuwezi kulisha uhitaji tumeshirikisha sekta binafsi ili kuweza kukidhi mahitaji mpaka sasa tumeshatoa idhini kwa kampuni 40 lakini kasi tuliyoitarajia haikuwa hivyo kasi imekuwa ni ndogo”,Amesema Gilbert.
Aidha ameongeza kuwa mpango wa TPDC ni kuhakikisha mpaka ifikapo mwisho wa mwaka huu wa fedha kuwa na vituo 13 zaidi ambavyo ni vipya tofauti na hivyo vitatu vilivyopo.
Akizungumzia mradi wa vituo vya kuhamushika(MOBILE CNG STATION) amesema huo ni moja ya miradi waliyokuwa nayo ambapo inahitajika magari sita la kuweza kutoa huduma hiyo hivyo tayari zabuni ilishatangazwa na kampuni nne za wazawa tayari zimejitokeza.
“Huu ni mpango wa muda mrefu kwani mpaka sasa mikoa iliyopitiwa na bomba letu ni mitatu hivyo hivi vituo sita tumevigawa katika mikoa ambapo 3 vitakuwa Dar es salaam,1 Morogoro ma 2 vitakuwa Dodoma kwa kuanzia”,Amesema.