WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka vijana wachangamkie fursa zinazotokana na maendeleo ya teknolojia katika kujipatia kipato na kushiriki kukuza Uchumi wa Taifa. Amesema kuwa vijana wanapaswa kutumia mitandao ya kidijitali kutafuta fursa za masoko na upatikanaji wa bidhaa ili kufanikisha malengo ya kuifanya Tanzania kuwa Taifa lenye maendeleo endelevu kupitia nguvu ya vijana na teknolojia.... Read More