Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mussa Kilakala amelaani vikali baadhi ya Tabia zinazofanywa na wafugaji ya kuwaachia watoto kwenda kuchunga mifugo hali ambayo husababisha migogoro ya wakulima na wafugaji
Akizungumza katika ziara yake katika kijiji Cha Mvuha DC Kilakala amesema kuwa wazazi wanapowaachia watoto kwenda kuchunga husababisha kuvamia Mashamba ya wakulima kwani wao wanafanya bila kuelewa na kusababisha wakulima kuanzisha vurugu Baada ya mazao yao kuliwa.
Amesema ni marufuku kwa mkulima au mfugaji kujiichukulia Sheria mkononi badala yake wanatakiwa changamoto zote zipelekewe kwenye vyombo vya Sheria ili iweze kuchukua hatua.
Amesema kitendo cha watoto kuchunga inawanyima haki kupata elimu hivyo Serikali itahakikisha jamii hiyo inaachana na utamaduni wa kutumikisha watoto kwenye shughuli mbalimbali
Kwa upande wake katibu wa chama cha wafugaji Wilaya ya Morogoro Emanuel Mselemu amesema wataendelea kutoa elimu Kwa wafugaji wengine ili kuacha kutumikisha watoto.
Amesema suala la kusomesha watoto linapewa kipaumbele na jamii hiyo tofauti na kipindi cha nyuma na wazazi wanapatia uelewa wa kufahamu umuhimu wa elimu
Mselemu amesema suala la Migogoro ya wakulima na wafugaji chama hicho linasimamia vyema Kwa kuhakikisha halijitokezi na kuleta madhara kati ya pande hizo mbili.
The post DC Morogoro Mussa Kilakala awataka wafugaji kuacha kutumikisha watoto first appeared on Millard Ayo.