Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
Mwenyekiti wa Washiriki wa mafunzo ya kozi ya ‘Sustainable and Inclusive Women Leadership and Management’
(SIWOLEMA) Training Program yaliyofanyila kuanzia tarehe 22 hadi 28 Septemba 2024, yamefungwa.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wahitimu Mwenyekiti wa Wahitimu wa mafunzo hayo Naomi Zegezege amesema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samis Suluhu Hassan juhudi anazofanya kuhakikisha wanawake wanajengewa uwezo ili waweze kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia serikalini, katika mashirika ya umma, sekta binafsi na hata katika shughuli mbalimbali za kujipatia kipato ilikuendeleza uchumi wa nchi yetu.
Zegezege amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazothamini mchango wa mwanamke katika uongozi na ngazi mbalimbali za kiutendaji na hivyo Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa maelekezo katika majukwaa mbalimbali yanayohusu mwanamke kuwa ni lazima wanawake wajengewe uwezo kupitia mafunzo mbalimbali yanatolewa na vyombo vyetu vya elimu au majukwaa mbalimbali ili waweze kugombea nafasi mbalimbali na pia kupewa majukumu makubwa ya kuongoza pale inapobidi.
Zegezege amesema kuwa tusipojifunza kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa kwanza Mwanamke Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla tutajifunza kutoka wapi tena?
Washiriki katika Mafunzo hayo wametoka katika Wizara mbalimbali ikiwemo Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Katiba na Sheria, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Halmashauri ya Mkoa wa Pwani, Mamlaka ya Mawasiliano, Benki ya NMB, Benki ya CRDB.
Washiriki hao wamejifunza masuala muhimu ya uongozi kwa upana mkubwa kuanzia maeneo muhimu yanayowezesha shughuli za serikali kufanyika bila kuingiliwa kama vile masuala ya Usalama wa Taifa tukianzia na ulinzi wa mipaka, na raia wake, umuhimu wa upatikanaji wa huduma za jamii.
” Tumejifunza hatua kubwa ambayo serikali imepiga katika kuinua uchumi wa kila mwananchi” amesema Zegezege .
Zegezege amesema kuwa “tumejifunza mambo mengi yaliyotujengea uwezo mkubwa katika uongozi ikiwemo kuongoza watu katika nafasi zetu, kujenga timu yenye nguvu ya umoja na utekelezaji wa maagizo ya serikali, masuala ya utawala bora, kuandaa mipango kazi, ukusanyaji wa fedha na utafutaji wa mapato, namna ya kujenga sura nzuri ya serikali kwa ujumla kupitia Taasisi zetu tunazozitumikia na namna ya kuwasiliana na kupashana habari
nidhamu eneo la kazi , uadilifu, masuala ya Itifaki za ndani na za Kimataifa, tumejifunza masuala ya majadiliano kuinua vipaji vya maafisa tunaowaongoza na kuwajengea uwezo wa kujiamini” amesema Zegezege.