DODOMA
Mahakama ya Hakimu Mkazi (Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki) imewahukumu Kifungo cha maisha gerezani na faini ya Tsh. Milioni 1 kila mmoja, washtakiwa Wanne baada ya kupatikana na hatia ya Makosa ya kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume na maumbile Binti Mkazi wa Yombo Dovya
Waliofungwa Maisha ni MT 140105 Clinton Damas, anayefahamika kama “Nyundo” kutoka JWTZ, Askari wa Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson maarufu “Machuche” na Amin Lema, anayejulikana pia kama “Kindamba
Katika kesi hiyo upande wa Jamhuri uliwasilisha Mashahidi 18 na vielelezo 12 kuthibitisha mashtaka dhidi ya Watuhumiwa hao.