Mtwara. Kampuni ya
michezo ya kubashiri ya betPawa imetumia jumla ya Sh 69.3 millioni
kukamilisha ujenzi na uboreshwaji wa zahanati ya kijiji cha Nangomba ya
mkoani Mtwara.
Fedha hizo zimetimika katika ujenzi, uboreshaji na
upanuzi wa zahanati hiyo kupitia programu ya Dream Maker yenye lengo la
kusaidia kutatua changamoto mbalimbali katika jamii nchini.
Meneja
Masoko kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya betPawa, Bi Borah
Ndanyungu amesema kuwa wanajisikia fahari kushiriki katika jamii hasa
sekta ya afya na kutatua tatizo hilo kwa kijiji cha Nangomba.
Bi
Ndanyungu alisema kuwa hatua ya kuboresha zahanati imetokana na maombi
yaliyowasilishwa na Afisa Tabibu, Bw Anania Muba kupitia program ya
Dream Maker ambayo mpaka sasa imetatua changamoto mbalimbali 20 katika
jamii,
“Uboreshwaji huo ni pamoja na kukarabati kuta
zilizoharibika, kuinua urefu wa jengo, kuongeza mihimili na kumalizia
kupiga plasta, kuweka milango, tiles, kupaka rangi kuta na kufunga
madirisha ya kisasa ya Aluminum,” alisema Bi Ndanyungu.
Alisema
kuwa Bw Muba aliwasiliana na betPawa kupitia mradi wa Dream Maker,
akitafuta usaidizi katika kukamilisha ukarabati wa kituo cha umma baada
ya maendeleo yake kukwama.
“Mpaka zaidi ya Sh500 milini
zimetumika kusaidia jamii kupitia program ya Dream Maker na fedha hizo
zimetumika kwa miezi 10. Programu ya Dream Maker ni mkakati wa kampuni
yetu katika kusaidia jamii.
Ni ndoto za upendo kama hizi
zinazotuhamasisha na kuendesha mradi wa Dream Maker kwa sababu tunajua
kwamba pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kudumu na chanya kwa kila
jamii kwa wakati mmoja,” alisema.
Kwa upande wake, Bw Muba alisema
kuwa ndoto yake kubwa ilikuwa kukamilisha ukarabati na upanuzi wa
kliniki yao ambayo inatoa huduma kwa wakazi zaidi ya 9,785.
“Jengo
tulilokuwa tukilitumia hapo awali lilikuwa katika hali mbaya na
halikuwa salama kutumika kama kituo cha afya. Nashukuru betPawa kwa
kufanya ndoto yangu kuwa kweli kwa kukubali ombi langu ndani ya muda
mfupi. Wakazi wa Ndangoma na maeneo jirani kwa sasa wanaweza kufurahia
huduma katika mazingira ya kisasa, salama na ya usafi,” alisema Bw Muba.
Kwa
upande wake, Diwani wa Nangomba, Bw Sijaona Athumani aliipomgeza
kampuni ya betPawa kwa kufanikisha mradi huo kutoa wito kwa kampuni
mbalimbali kuiga mfano wa kamupuni hiyo kwa changamoto katika jamii bado
ni nyingi.
“Nifuraha kuweza kuona zahanati hii itahudumia idadi
ya wananchi wasiopungua 9,785 wakitokea sehemu mbalimbali hapa
kijijini. Naishukuru betPawa kwa kutufanikishia ujenzi na uboreshwaji wa
kituo hiki. Bw Muba ameonyesha uzalendo wake kwa wakazi wa Ndangoma,
naomba kila mmoja aige mfano wake,” alisema Bw Athumani.