WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni imewataka wenye viwanda na makampuni kusajili bidhaa zao kwa lengo la kupata masoko ndani na nje ya nchi katikà Maonesho ya pili ya Kimataifa ya Viwanda yanayofanyika kwenye viwanja vya sabasaba Jijini Dar es Salaam kwaajili ya kupata huduma.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho hayo leo Oktoba 1, 2024 Jijini Dar es Salaam, Afisa Leseni BRELA, Ndeyanka Mbowe amesema wapo hapo kwa ajili ya kusajili viwanda na biashara na kutoa elimu kwa jamii ijue umuhimu wa kusajili bidhaa zao.
Aidha Mbowe amesema toka mwaka 2018 walianza shughuli za usajili kwenye viwanda huku wakiwa wanaiendesha BRELA kisasa.
Amesema kuwa BRELA imejiwekea mikakati mbalimbali ikiwemo kutoa elimu kwa jamii na kujua umuhimu wa kusajili viwanda kampuni.
“Ukisajili kampuni au kiwanda unakuwa na nafasi kubwa ya kushiriki maonesho ya ndani na nje ambayo yanatoa fursa ya kutangaza bidhaa yako,”alisema .