Takriban watu sita waliuawa katika shambulio la anga la Israel kwenye jengo la ghorofa katikati mwa Beirut, Wizara ya Afya ya Lebanon imesema.
Watu wengine 11 walijeruhiwa katika shambulio hilo huko Beirut mwishoni mwa Jumatano, wizara ilisema.
Shambulio hilo lilianzisha moto katika ghorofa katika jengo la ghorofa nyingi katika wilaya ya makazi ya Bashoura, karibu na makao makuu ya Umoja wa Mataifa, ofisi ya waziri mkuu na bunge.
Wakaazi waliripoti harufu kama ya salfa kufuatia shambulio hilo, na Shirika la Habari la Taifa la Lebanon (NNA) liliishutumu Israel kwa kutumia mabomu ya fosforasi yaliyopigwa marufuku kimataifa.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu siku za nyuma yameishutumu Israel kwa kutumia makombora nyeupe ya fosforasi katika miji na vijiji vilivyokumbwa na vita kusini mwa Lebanon.
The post Shambulio la Israel kwenye jengo la ghorofa katikati mwa Beirut laua watu sita first appeared on Millard Ayo.