Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa mapema leo amefika kwenye Chuo cha Ukamanda na Unadhimu – Tanzania, kwa ajili ya kutoa muhadhara kwa Maafisa Wanafunzi wa Kozi ya Ukamanda na Unadhimu Kundi la 39/2024.
Muhadhara unahusu namna ambavyo Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii yanavyochangia katika kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi.
Aidha, Uongozi wa Chuo umempatia zawadi Waziri Mchengerwa zenye kubeba taswira ya Chuo ikiwa ni ishara ya shukrani kwake kwa kukubali mwaliko na kuwasilisha mada ambayo imewajengea uelewa na ufahamu mkubwa Wanafunzi kuhusu mada husika.