Waziri wa Viwanda na Biashara Bw Selemani Jafo akizungumza wakati wa kufunga maonesho ya pili ya kimataifa ya viwanda Tanzania (Tanzania International Manufacturers -TIMEXPO 2024) yaliyoandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) chini ya uratibu wa kampuni ya Radian Limited. Maonyesho hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Sabasaba.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) Bi Latifa Khamis akizungumza wakati wa kufunga maonesho ya pili ya kimataifa ya viwanda Tanzania (Tanzania International Manufacturers -TIMEPO 2024) yaliyoandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) chini ya uratibu wa kampuni ya Radian Limited. Maonyesho hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Sabasaba.
Makamu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Bi Mariam Ditopile Mzuzuri, akizungumza wakati wa kufunga maonesho ya pili ya kimataifa ya viwanda Tanzania (Tanzania International Manufacturers -TIMEPO 2024) yaliyoandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) chini ya uratibu wa kampuni ya Radian Limited. Maonyesho hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Sabasaba.
Waziri wa Viwanda na Biashara Bw Selemani Jafo (wa sita kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kutembelea banda la Kampuni ya Airplanes Africa Limited (AAL) na kujionea ndege ya kwanza kutengenezwa Tanzania aina ya Skyleader 600 kupitia maonesho ya pili ya kimataifa ya viwanda Tanzania (Tanzania International Manufacturers -TIMEPO 2024) yaliyoandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) chini ya uratibu wa kampuni ya Radian Limited. Maonyesho hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Sabasaba.
Washiriki mbalimbali wakimzikiliza Waziri wwa Viwanda na Biashara Bw Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati wa kufunga maonesho ya pili ya kimataifa ya viwanda Tanzania (Tanzania International Manufacturers -TIMEPO 2024) yaliyoandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) chini ya uratibu wa kampuni ya Radian Limited. Maonyesho hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Sabasaba.
Waziri wa Viwanda na Biashara Bw Selemani Jafo (kushoto) akiwa ndani ya ndege ya kwanza kutengezwa Tanzania aina ya Syleader 600 wakati wa kufunga maonesho ya pili ya kimataifa ya viwanda Tanzania (Tanzania International Manufacturers -TIMEPO 2024) yaliyoandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) chini ya uratibu wa kampuni ya Radian Limited. Maonyesho hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Sabasaba.
………………..
Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda na Biashara Bw Selemani Jafo amesema kuwa ifikapo mwaka 2030, kila mkoa unatakiwa kuwa na viwanda vikubwa vitatu kwa lengo la kuleta mapinduzi ya sekta hiyo, kuongeza ajira na kuinua uchumi.
Bw Jafo amesema hayo wakati wa kufunga maonyesho ya pili ya kimataifa ya viwanda Tanzania (Tanzania International Manufacturers -TIMEXPO 2024) yaliyoandaliwa naShirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) chini ya uratibu wa kampuni ya Radian Limited.
Alisema kuwa mbali ya viwanda vitatu vikubwa, mikoa pia inatakuwa kuwa na viwanda vya kati vitano na vidogo visivyongua 30 kwa lengo la kuongeza soko la ajira si chini ya watu 185,000.
“Mpango huu wa kuleta maendeleo ya viwanda na biashara unatarajia kuanza mwakani ambapo kuanzia sasa, kila mkoa unatakiwa kutenga maeneo ya kujenga viwanda hivyo ili kuufanisha,” alisema Bw Jafo.
Alifafanua kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya vwanda, biashara na nyinginezo.
Alisema kuwa serikali ina malengo ya kuendeleza nchi kwa kuwapatia Watanzania fursa nyingi hukuakitoa wito kwa wamiliki wa viwanda kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kupata wateja wengi na kuleta ushindani katika masoko ya ndani, kikanda na kimataifa.
Kwa mujibu wa Bw Jafo, serikali inaendelea kuimarisha Diplomasia ya Uchumi na kuwataka wenye viwanda na wafanyabiashara kuchangamkia fursa zinazopatikana bila kusahau kuwa biashara duniani ni huria na yenye ushindani.
“Hivyo naomba kusisitiza umuhimu wa wazalishaji wetu kuzalisha bidhaa zenye ubora na zinazoendana na matakwa ya soko, natoa wito kwa Taasisi zetu mbalimbali za serikali kuwa wasimamizi waelekezi na siyo wasimamizi wakwamishaji hususan kwa viwanda.
Nawahakikishia wenye viwanda na wazalishaji wote kuwa wizara yangu itaendelea kusimamia sekta hii katika kuhakikisha kuwa azma ya serikali ya kukuza na kuendeleza sekta ya wiwanda nchini inafikiwa,” alisema.
Bw Jafo pia alitoa wito kuendelea kujenga ushirikiano kwa serikali na taasisi zake mbalimbali katika kufanya majadiliano ili kuhakikisha kuwa changamoto mbalimbali zinazowakabili wawekezaji zinatatuliwa.
Katika hatua nyingine, Bw Jafo alisema kuwa serikali inakuja na mpango mkubwa wa kufufua viwanda ambavyo havifanyi uzalishaji kwa sasa ukiwa kutoa fursa kwa wawezaji binafsi.
“ Mfano kuna kiwanda kikubwa cha korosho Tunduru na kusababisha ajira zaidi ya 604 kupotea. Pia kuna viwanda zaidi ya 11 Nachingwea, Lindi na Mtwara ambavyo kwa sasa havifanyi uzalishaji. Nawaomba wawekezaji kuwa tayari kuwekeza katika viwanda ambavyo serikali itavitangaza kuitaji wawekezaji wapya,” alisema.
Pia Bw Jafo aliziomba taasisi za kibenki kupunguza riba ili kuwazesha wawekezaji wa ndani kupata mitaji.
Alisema kuwa wawekezaji wengi hawana mtaji wa kutosha na hivyo kutoa wito kwa taasisi za fedha kunguza riba na kuwavutia wawezaji wengi kupata mitaji na kuiwezesha nchi kuwa na viwanda vingi na kukuza biashara na uchumi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) Bi Latifa Khamis alisema kuwa maonyesho hayo yamefanikiwa kutokana na washiriki kuongezeka kutoka 79 na kufikia washiriki 257.
“Nitoe wito kwa wentye viwanda kushiriki maonesho yanayokuja ambayo tunaamini yatakuwa na mafanikio zaidi,” alisema Bi Khamis.
Wakati huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), Bw Leodgar Tenga alitoa wito kwa wenye viwanda wa jijini Dar es Salaam mikoa mingine kushiriki katika maonesho yajao ili kupanua wigo wa biashara na kupata washirika.