Paris Saint-Germain bado wana matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah, The Sun linaripoti.
Salah, 32, mkataba wake unamalizika Anfield mwishoni mwa msimu huu, lakini PSG wanaamini kuwa bado anaweza kushindana katika kiwango cha juu cha soka la Ulaya kwa angalau miaka mitatu mingine.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri, ambaye tayari ana mabao sita na asisti tano msimu huu, alifichua mwezi uliopita kwamba huenda akacheza katika msimu wake wa mwisho kwa Liverpool huku kandarasi yake ikitarajiwa kumalizika mwishoni mwa kampeni.
Alisema Septemba 1: “Hakuna mtu katika klabu ambaye amezungumza nami kuhusu mikataba, kwa hivyo ni sawa nitacheza msimu wangu wa mwisho na tutaona mwishoni mwa msimu. Si juu yangu.”
The post Salah bado anasakwa na PSG first appeared on Millard Ayo.