Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mradi wa Ujenzi wa Bweni katika Shule ya Sekondari Kibasila akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Temeke, Mkoa wa Dar es salaam, Oktoba 5, 2024. Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Abbas Mtemvu, Mbunge wa Mbagala, Abdallah Chaurembo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila na wa pili kulia ni Mbunge wa Temeke, Dorothy Kilave. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe alipozindua Mradi wa Ujenzi wa Bweni katika Shule ya Sekondari Kibasila akiwa katika ziara ya Wilaya ya Temeke mkoani Dar es salaam, Oktoba 5, 2024. Wengine kutoka kushoto ni Mbunge wa Mbagala, Abdallah Chaurembo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Abbas Mtemvu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila na kulia ni Mbunge wa Temeke, Dorothy Kilave. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Huduma za Uhandisi Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Erick Madinda kuhusu Ujenzi, Upanuzi na Ukarabati wa Daraja na Barabara ya Mivinjeni na Bandari One jijini Dar es salam. Alikuwa katika ziara ya kikazi wilayani Temeke Mkoa wa Dar es salaam, Oktoba 5, 2024. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salam, Abbas Mtemvu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha kutoridhishwa na ukaribu uliofanywa katika ujenzi wa Hospitali ya Zakhem Mbagala jijini Dar es Salaam na kituo cha Mabasi ya Mwendo Kasi, alipokagua ujenzi wa Hospitali hiyo. Alikuwa katika ziara ya kikazi wilayani Temeke Mkoa wa Dar es salaam, Oktoba 5, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Muonekano wa Bweni la Shule ya Sekondari Kibasila mkoani Dar es salaam ambalo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alizindua ujenzi wake akiwa katika ziara ya Wilaya Temeke, Oktoba 5, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)