Na Mwandishi Wetu Michuzi Tv
TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) kwa kushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) imekuwa Mwenyeji wa mkutano wa Mafunzo ya WMO kwa wataalamu wa hali ya hewa kutoka nchi Wanachama wa WMO Kanda ya Afrika Mashariki na Kaskazini.
Lengo la mkutano ni kuwajengea uwezo wataalamu wa Hali ya Hewa wanaofanya kazi katika vituo hivyo vya “WMO Regional WIGOS Centres (RWCs)” vya kanda ya Afrika Mashariki na Kaskazini Afrika.
Akifungua mafunzo hayo yanayofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheratons, yaliyoanza leo Oktoba 7 hadi 11, 2024, Mgeni rasmi na Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Mhe.
“Suala muhimu kwa Taasisi za Hali ya Hewa za Afrika ni kuimarisha upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa zenye ubora kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi,
… hivyo mafunzo haya yatasaidia kuboresha zaidi shughuli zinazofanywa ikiwa ni pamoja na kuboresha mtandao wa kubadilishana data ili kuboresha utabiri wa matukio ya hali mbaya ya hewa katika nchi wanachama wa WMO”. Amesema Jaji Mshibe
Aidha, Jaji Mshibe ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwekeza katika uboreshaji wa miundo mbinu ya huduma za hali ya hewa.
Pia Jaji Mshibe amewashukuru WMO na washirika wengine kwa jitihada zao za kuimarisha huduma za hali ya hewa barani Afrika, ikiwemo kuanzisha mfuko wa uwezeshaji wa huduma za uangazi wa hali ya hewa ambapo kupitia jitihada hizo, kiasi cha dola za kimarekani milioni tisa zimeidhinishwa kuboresha huduma za hali ya hewa nchini Tanzania.
Awali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Mwakilishi wa kudumu wa WMO, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a, ameeleza umuhimu wa kuimairsha uangazi na kuongeza upataikanaji wa data kwa ajili ya kuimairsha utoaji wa tahadhari za matukio ya hali mbaya ya hewa na kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa. Aidha Dkt. Chang’a ameeleza kuwa Tanzania kupitia TMA imejipanga kuendelea kushiriki katika kuongoza na kuwa kinara katika baadhi ya jitihada za kuimarisha huduma za hali ya hewa Barani Afrika.
“ Tumejiandaa vyema kuwa mwenyeji wa Mkutano huu mkubwa wa Kikanda, na pia kama mwenyeji wa Kituo cha mfumo wa Kidunia wa kufuatilia vituo vya uangazi wa hali ya hewa kwa nchi za Afrika Mashariki” alisema Dkt. Chang’a.
TMA itawasilisha mada zenye kueleza uzoefu wake katika utekelezaji wa jukumu hilo.
Kwa upande wake, Mwakilikishi kutoka WMO amesema kumekuwa na changamoto ya matukio mbalimbali ya Hali mbaya ya Hewa hivyo ushirikiano wetu utasaidia katka kutoa tahadhari za mapema juu ya matukio ya Hali mbaya ya Hewa na tahadhali za mapema”.Amesema, Abubakari Babiker
Washiriki wa mkutano huo wametoka Taasisi za Hali ya Hewa za nchi za Tanzania, Tunisia, Algeria, Egypt, Sudan, South Sudan, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Ethiopia, Djibouti, Madagascar, Comoros, Sychelles, Mauritius, Morocco, Afrika Kusini na waalikwa kutoka Oman na Sekretarieti ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani.