Kulwa James Kasuka, Mhasibu Mwandamizi kutoka Bodi ya Bima ya Amana DIB kulia akitoa zawadi ya mifuko kwa wananchi waliotembelea kwenye banda la DIB katika maonesho ya teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geite.
Afisa kutoka Bodi ya Bima ya Amana (DIB) Careen Max akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliotembelea katika banda hilo.
…………….
Bodi ya Bima ya Amana (DIB) imewahimiza wananchi wa Geita kufanya biashara bila wasiwasi, kwani sekta ya fedha nchini iko imara na ina utulivu.
Hayo yamesemwa leo, Oktoba 8, 2024, na Kulwa James Kasuka, Mhasibu Mwandamizi kutoka Bodi ya Bima ya Amana, wakati akizungumza oktoba 8, 2024 kwenye maonesho ya 7 ya teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita
Kasuka ameeleza kuwa benki zote nchini zinalazimika kisheria kukatia bima amana za wateja wao. Alisema kuwa endapo benki itafungwa au kufilisika, wananchi watafidiwa kupitia bima ya amana, hivyo hawana sababu ya kuwa na wasiwasi wowote.
“Endapo benki zitafungwa au kufilisika, wananchi watapokea fidia. Kiwango cha fidia ni kati ya shilingi 1 hadi milioni 7 na laki 5, na fedha zinazozidi kiwango hicho zitasubiri mchakato wa ufilisi,” alisema Kasuka.
Aidha, Kasuka alibainisha kuwa viwango hivyo vimefanyiwa tafiti, na takriban asilimia 98 ya wateja wa benki wana amana kati ya shilingi 1 hadi milioni 7 na laki 5. Alifafanua kuwa kiwango hiki kinaweza kuongezeka kadri uchumi unavyoendelea kukua.
“Kwa mfano, hapo awali kiwango cha fidia kilikuwa milioni 1 na laki 5, lakini baada ya kuona uchumi umekua na watu wameongeza kuweka amana zaidi benki, tumeongeza kiwango hicho,” alisisitiza Kasuka.
Kasuka aliongeza kuwa asilimia kubwa ya wateja wanaofidiwa ni wale walio na amana ndogo, huku wateja wenye kiasi kikubwa cha fedha, kama vile milioni 300 au zaidi, wakiwa wachache.
Aliwahimiza wadau wa benki kuendelea kuweka pesa zao kwenye benki kwani ni salama, na sekta ya fedha nchini imeendelea kuwa thabiti.
Miongoni mwa kazi muhimu za Bodi ya Bima ya Amana ni kuhamasisha utunzaji wa amana na kuimarisha imani kwa sekta ya kifedha: DIB inatekeleza kampeni za kuhamasisha wananchi kuweka akiba katika taasisi za kifedha zilizosajiliwa na kuhakikishiwa na bima ya amana, kwa lengo la kuongeza imani katika mfumo wa benki.
Vilevile Kufanya ufuatiliaji wa taasisi za kifedha ambapo Bodi ya DIB inahakikisha kuwa benki na taasisi za kifedha zinafuata miongozo ya kisheria inayohusiana na usimamizi wa amana za wateja, na pia inafanya ukaguzi wa mara kwa mara.
Jukumu lingine ni kuwa DIB ina wajibu wa kutoa elimu kwa umma kuhusu mfumo wa bima ya amana, faida zake, na namna inavyowalinda wateja wa benki dhidi ya hasara zinazoweza kujitokeza kwenye sekta ya kifedha.
Amesema Bodi ya Bima ya amana DIB itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya fedha ili kuhakikisha wateja wanapata huduma bora na salama kupitia mifumo ya amana yenye uhakika na