Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, wakiwa katika picha baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania uliodumu kwa miaka 60 sasa. Mhe. Dkt. Nchemba ameishukuru China kwa kufikia hatua za mwisho za kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR unaendelea hivi sasa kwa kipande cha tano cha kuanzia Mwanza hadi Isaka na kuahidi kuyafanyiakazi maombi mengine ya fedha za kujenga kipande cha sita kinachoanzia Tabora hadi Kigoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa tatu kulia), akiongoza kikao na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian (hayupo pichani),, kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania uliodumu kwa miaka 60 sasa, na ameishukuru China kwa kufikia hatua za mwisho za kufadhili ujenzi wa Reli ya kisasa ya SGR unaendelea hivi sasa kwa kipande cha tano (kuanzia Mwanza hadi Isaka) na kuahidi kuyafanyiakazi maombi mengine ya fedha kwa ajili ya kujenga kipande cha sita kinachoanzia Tabora hadi Kigoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati wa kikao na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian (hayupo pichani),, kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania uliodumu kwa miaka 60 sasa, na ameishukuru China kwa kufikia hatua za mwisho za kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR unaendelea hivi sasa kwa kipande cha Tano cha kuanzia Mwanza hadi Isaka na kuahidi kuyafanyiakazi maombi mengine ya fedha kwa ajili ya kujenga kipande cha Sita kinachoanzia Tabora hadi Kigoma.
Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, akizungumza wakati wa kikao na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania uliodumu kwa miaka 60 sasa, na amesema kuwa nchi yake inauchukulia uhusiano wake na Tanzania kiuchumi, kiutamaduni na kijamii kuwa ni wa kipekee na kwamba maelekezo ya Kiongozi wa nchi hiyo Mheshimiwa XI Jinping ni kwamba anataka uhusiano huo uwe wa mfano na kielelezo barani Afrika.
Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, akiwa na ujumbe kutoka ubalozi wa china nchini, wakimsikiliza Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), wakati wa kikao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania uliodumu kwa miaka 60 sasa. Kushoto ni Bw. Chu Kun na kulia ni Katibu wa Balozi, Bi. Ma Shukun. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)
………
Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameishukuru China kwa kufikia hatua za mwisho za kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR unaendelea hivi sasa kwa kipande cha tano cha kuanzia Mwanza hadi Isaka na kuahidi kuyafanyiakazi maombi mengine ya kipande cha sita kinachoanzia Tabora hadi Kigoma.
Dkt. Nchemba ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini, Mheshimiwa Chen Mingjian, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania uliodumu kwa miaka 60 sasa.
Dkt. Nchemba alisema kuwa Mradi wa Reli ya Kisasa ni muhimu kwa uchumi na maendeleo ya Watanzania na kwamba ujumbe wa Mheshimiwa Balozi Chen kwamba China kupitia taasisi zake inakamilisha taratibu za ndani za kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo umepokelewa kwa mikono miwili na Serikali.
Kwa upande wake, Balozi wa China hapa nchini, Mheshimiwa Chen Mingjian, amesema kuwa nchi yake inauchukulia uhusiano wake na Tanzania kuwa ni wa kipekee na kwamba maelekezo ya Kiongozi wa nchi hiyo Mheshimiwa XI Jinping ni kwamba anataka uhusiano huo uwe wa mfano na kielelezo barani Afrika.
Alisisitiza kuwa maombi ya Tanzania ya kupata fedha kwa ajili ya kipande cha tano na mengine ya kutaka ufadhili wa ujenzi wa kipande cha 6 yamepokelewa na kwamba uamuzi wake utatolewa hivi karibu baada ya mambo machache yanayofanyiwakazi kukamilika.
Aidha, alieleza kuwa mpango wa miaka mitatu wa China wa ushirikiano kati yake na nchi za Afrika (FOCAC), umeitengea Tanzania kiasi kikubwa cha fedha ambazo zitaelekezwa katika miradi inayogusa masuala ya uchumi wa kijani, biashara na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).