Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank of Africa (UBA), Bw. Gbenga Makinde, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo ameishukuru Benki hiyo kwa kuwa tayari kuendelea kushirikiana na Serikali katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Katikati), alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank of Africa (UBA), Bw. Gbenga Makinde (Kulia), katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo ameishukuru Benki hiyo kwa kuwa tayari kushirikiana na Serikali katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere. Kushoto ni Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni, Bw. Japhet Justine.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati wa kikao chake na Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank of Africa (UBA), Bw. Gbenga Makinde (hayupo pichani), baada ya kukutana na kufanya mazungumzo, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo ameishukuru Benki hiyo kwa kuwa tayari kuendelea kushirikiana na Serikali katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere.
Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank of Africa (UBA), Bw. Gbenga Makinde, akizungumza wakati wa kikao chake na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), wakati walipokutana na kufanya mazungumzo, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo ameeleza kuwa Benki yake imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika kutekeleza baadhi ya miradi yake ya kimkakati ikiwemo Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere na ameahidi kuwa Benki hiyo iko tayari kushirikiana moja kwa moja na Serikali kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi husika.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank of Africa (UBA), Bw. Gbenga Makinde, wakiwa katika picha ya pamoja baada kukutana na kufanya mazungumzo, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ikiwemo ushirikiano wa Benki hiyo kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam).
……………
Na. Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameishukuru United Bank of Africa (UBA), kwa kuwa tayari kushirikiana na Serikali katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo.
Dkt. Nchemba, ametoa shukrani hizo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank of Africa (UBA), Bw. Gbenga Makinde, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa Serikali inatekeleza miradi mingi ya kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake na kuialika Benki hiyo kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo reli na umeme.
Kwa upande wake, Bw. Makinde, ameeleza kuwa Benki yake imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika kutekeleza baadhi ya miradi yake ya kimkakati ikiwemo Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere, kwa kuwawezesha kifedha wakandarasi wanaojenga mradi huo na kwamba hivi sasa Benki hiyo iko tayari kushirikiana moja kwa moja na Serikali kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi husika.
UBA ni Taasisi ya fedha ambayo iko nchini kwa miaka 15 na ina matawi zaidi ya 20 katika nchi za Afrika, na baadhi ya nchi za ulaya na Marekani.